RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH.JAKAYA KIKWETE AKITANGAZA BARAZA LA MAWAZIRI IKULU JIJNI DAR ES SALAAM Hili ni baraza jipya la mawaziri lililotangazwa na mh.JK Mrisho tarehe 24.November 2010, 1:58 pm ikulu jijini Dar es salaam,baraza hilo ambalo limekuwa na mabadiliko kadha wa kadha ambapo mh.raisi amebadilisha maadhi ya mawaziri na manaibu mawaziri katika serekali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kama inavyoonekana hapo chini,katika mabadiliko haya mh.raisi amepangua na kupalangiza mawaziri kikubwa zaidi ameongeza majukumu katiaka baadhi ya wizara na kupunguza majukumu katika baadhi ya mawaziri,
Hili ni baraza jipya la jamhuri ya muungano wa Tanzania na watanzania wengi wa naamini kuwa gurudumu lao la maendeleo litakuwa na speed kubwa ilikuhakikisha kuwa kuna kuwa na maendeleo ya kijamii,kiuchumi halikadhalika na Nyanja zingine katika nchi kwa ujumla
1. Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Mathias Chikawe
2. Ofisi ya Rais – Mahusiano na Uratibu: Stephen Wassira
3.Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma Hawa Ghasia
4. Ofisi ya Makamu wa Rais – ( Muungano): Samia Suluhu
5. . Ofisi ya Makamu wa Rais – (Mazingira) Dr. Terezya Luoga Hovisa
6. Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge): William Lukuvi
7. Uwekezaji na Uwezeshaji Dr. Mary Nagu
8. Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Huruma Mkuchika
Naibu: Aggrey Mwanri
Naibu: Kassim Majaliwa
9. Wizara ya Fedha Mustapha Mkulo
Naibu: Gregory Teu
Naibu: Pereira Ame Silima
10. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Shamsi Vuai Nahodha
Naibu: Balozi Khamis Suedi Kagasheki
11. Wizara ya Katiba na Sheria Celina Kombani
12. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard K. Membe Naibu: Mahadhi Juma Mahadhi
13 . Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dr. Hussein Ali Hassan Mwinyi
14. Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dr. Mathayo David Mathayo
Naibu: Benedict Ole Nangoro
15. Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mnyaa Mbarawa
Naibu: Charles Kitwanga
16. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka Naibu: Goodluck Ole Madeye
17. Wizara ya Maliasili na Utalii Ezekiel Maige
18. Wizara ya Nishati na Madini William Mganga Ngeleja 1. Adam Kigoma Malima
19. Wizara ya Ujenzi Dr. John Pombe Magufuli
Naibu: Dr. Harrison Mwakyembe
20. Wizara ya Uchukuzi Omari Nundu
Naibu: Athumani Mfutakamba
21. Wizara ya Viwanda na Biashara Dr. Cyril Chami
Naibu: Lazaro Nyalandu
22. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr. Shukuru Kawambwa
Naibu: Philipo Mulugo
23. Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Haji Hussein Mpanda
Naibu: Dr. Lucy Nkya
24. Wizara ya Kazi na Ajira Gaudensia Kabaka Makongoro Mahanga
25. Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Sophia Simba
Naibu: Umi Ali Mwalimu
26. Wizara ya Habari, Vijana na Michezo Emmanuel John Nchimbi
Naibu:Dr. Fenella Mukangara
27. Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel John Sitta
Naibu Dr. Abdallah Juma Abdallah
28. Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Prof. Jumanne Maghembe
Naibu: Christopher Chiza
29. Wizara ya Maji: Prof. Mark James Mwandosya
Naibu: Eng. Gerson Lwinge
Ngugu wasomaji wa blog hii ya jamii,hiyo ni list ya mawaziri ambao sisi kama wa Tanzania tunaamini kuwa baraza hili litaleta mabadiliko makubwa katika nchi yetu ya Tanzania na kuhakikisha kuwa kama kuna nchi tano au mbili katika Afrika basi Tanzania iwe ni mojawapo kati ya hizo,nasema hayo kwa sababu gani?,katika nchi ya Tanzania kuna kila aina ya malighafi ambayo ni muhimu kwa maendeleo,mfano;katika nchi zinazoongoza kwa uchimbaji wa dhahabu Tanzania ni nchi mojawapo kati ya hizo,ukiangalia upande wa madini ya thamani ya dimond,Tanzania nayo ni nchi inayotisha katika utoaji wa madini hayo,lakini pia Tanzania ni nchi ya kwanza na ni nchi inayoongoza kwa uzalishaji wa madini ya thamani ya Tanzanite yanayopatikana katikamji wa Arusha nchini Tanzania
Tanzania ni nchi pia inayomiliki mafuta katika ukanda wa bahari ya hindi kuanzia dar es salaam mpaka Zanzibar lakini pia kuna gesi asili inayopatikana katika maeneo hayohayo yenye mafuta kwa sababu sehemu yoyote yenye mafuta basin na gesi inapatikana hapo,hizo ni baadhi ya malghafi chache ambazo ambazo zinapatika na katika nchi hii nzuri na yenyekuvutia ya Tanzania.
Sasa ni mafikirio yetu sisi kama watanzania kuwa baraza hilo la mawaziri lililotangazwa na mh jk litakuwa likituweka mbele watanzania kwa kuhakikisha kuwa malighafi hizi zinatumiwa ipaswavyo bila kuharibiwa au kutapanywa na mafisadi kama ilivyokuwa klatika kipindi kilichopita na vingine vyote,tunaamini kuwa baraza hili la mawaziri litahakikisha kuwa watanzania wote wanakuwa salama kwa kuimarisha ulinzi wan chi ndani na nje kwa maana ya kuimarisha majeshi yote ya ulinzi na usalama kama vile jwtz polivce Tanzania na mengine pia.
Lakini serekali nzuri ni ile ambayo inahakikisha kuixwa kunakuwa namaendeleo endelevu kwananchi wake wote kwa kufanya mambo kama vile kuhakikisha kuwa kunakuwa na huduma zote za ja mii kwa wananchi wote,lakini pia kujaribu kutoa mikopo kwa wananchi tena kwa masharti nafuu ili kuweza kuongeza uzalishaji ndani ya nchi,pamoja na njia mbadala nyinginezo serekali hii tunayoiamini inaweza kutuletea maendeleo katika Tanzania yetu